Friday, April 3, 2015

Oliver Giroud, Arsene Wenger kwenye tuzo hii ya ligi kuu England

giroud 
Chelsea ndio vinara wa ligi kuu ya England kwa kuongoza huku ikiwa na pointi 67 mkononi lakini unaambiwa licha ya Arsenal kushikilia nafasi ya tatu imeweza kufanya vizuri na kuibuka na tuzo za kila mwezi kwa kufanya vizuri.
Mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi katika ligi kuu ya England baada ya kazi yake nzuri akiwa na kikosi hicho.
Giroud raia wa Ufaransa amepata tuzo ikiwa ni ya 16 tangu kuanza kutolewa.
wenger 
Naye kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa ligi kuu ya England kwa mwezi Machi ikiwa ni mara ya 14 kwake kutwaa tuzo hiyo.

Saturday, March 28, 2015

Baada ya ugomvi wa Madirector wawili wa Tanzania, haya manne ni kutoka kwa Adam Juma.

 

ad 5 
Anayo heshima yake kama Director wa video mkongwe kwenye kizazi cha Bongofleva ambae baada ya kuona maneno yakiendelea kurushwa kati ya Madirector wawili kwenye kizazi hikohiko, yani Nisher na Hanscana, Adam ameamua kutoa maneno yake kama kaka.

Kupitia page yake ya Instagram Adam aliweka hii picha hapa chini na kuandika >>> ‘Hizi vita za katika sanaa za kijinga sana, hazileti maendeleo bali chuki tu, vita kati ya madirector sio jambo la kushangilia hata kidogo, kwani mtu ukiwa wa kwanza wa pili maana yake nini?
‘Mnapoteza urafiki kwa umaarufu wa siku mbili, kitu hiki kilifanyika kwa Pfunk na Mj, then dunga na mapigo then lamar, wako wapi hawa watu ambao ndio mngongo wa mziki, ukiwaangalia hawa maproducer wote ni wakali ila ujinga ndio umesabisha ubishani usiokua na maendeleo’
Kwenye sentensi ya tatu akaandika >>> ‘Tujifunze kupenda na kuangalia style za wenzetu sio kwa lengo la kusema nani ni mkali au nani ni wa kwanza, kwa nia hiyo tutakuza sanaa, sijawahi hata siku moja kufikiria kwamba nimfunike mtu flani au niwe on top, bali nafanya kwa kadri ya uwezo wangu kuwa tofauti, mengine nawaachia watazamaji’
‘Sitaki kufananishwa na mtu yoyote yule kwa uzuri wala ubaya, kama hujaelewa nachokifanya nunua camera fanya wewe, nawaonya nyie mnaogombana mkiwa mmesahau mlipotoka, UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU. Hakuna aliyebora kati yetu wote tunaudhaifu wetu’
ad 1
ad 2
ad 3
ad 4